Mambo saba ambayo ni marufuku Ethiopia

Ghasia za hivi karibuni zimejiri kufuatia mauaji ya watu 55 katika tamsaha la kidini la Oromia Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ghasia za hivi karibuni zimejiri kufuatia mauaji ya watu 55 katika tamsaha la kidini la Oromia

Serikali ya Ethiopia imetangaza miezi sita ya hali ya tahadhari kufuatia wimbi ambalo halikutarajiwa la maandamano na ghasia.

Wanaharakati katika eneo la Oromia wamekuwa wakifanya maandamano tangu November mwaka jana, na waandamanaji kutoka eneo la Amhara wamejiunga kati.

Vifo vya watu 55 katika tamasha la kidini la Oromo mnamo Oktoba 2 yalisababisha ghasia kuzuka upya, ikiwemo kulengwa kwa biashara za raia wa mataifa ya nje.

Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanasema watu 500 wamefariki katika maandamano hayo kwa jumla na wiki iliopita waziri mkuu Hailemariam Desalegn amesema huenda idadi hiyo ikawa ya sawa.

Hali hiyo ya tahadhari ilitangazwa mapema mwezi huu lakini serikali sasa imeeleza wazi ina maana gani kihalisia:

Hizi ndio baadhi ya marufuku:

1. Mitandao ya kijamii

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanaharakati wametumia simu zao kusambaza taarifa kuhusu maandamano yao

Hakuna ruhusa kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter, kuwasiliana na serikali inayowaita "vikosi vya nje". Jaribio lolote la kuwasiliana na "makundi ya kigaidi na makundi yanayopinga amani yanayotajwa kuwa ya kigaidi" ni marufuku.

Waandamanaji wametuma ujumbe na video walizo rekodi kwa simu zao katika mitandao ya kijamii na mitandao inayoendeshwa na raia wa Ethiopia walio katika nchi za nje.

Serikali imezishutumu Eritrea na Misri kwa kuchochea maandamano hayo.

2. Vyombo vya habari

Huwezi kutazama vituo vya Esat na OMN vya televisheni, vilivyo na makao yake nje ya nchi. Serikali imezitaja kumilikiwa na 'makundi ya kigaidi'.

3. Maandamano

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kumeshuhudiwa maandamano katika miezi ya hivi karibuni

Huwezi kupanga mandamano shuleni au katika chuo kikuu unakosoma, na hakuna ruhusa ya kuwa mfuasi wa kampeni ya kisiasa ambayo huenda 'ikazusha ghasia, chuki, na ukosefu wa imani miongoni mwa raia'.

4. Ishara

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanariadha Feyisa Lilesa alikunja mikono hewani katika mashindano ya Olimpiki mwaka huu - ishara ya maandamano ya Oromo inayotambulika kote duniani

Huwezi kuonyesha ishara ya kisiasa, kama kukunja mikono juu ya kichwa au kuwasilisha ujumbe wa kisiasa kwa umma 'bila ya ruhusa'.

Ishara hiyo ya kukunja mikono imetumika pakubwa katika maandamano ya Oromo na pia katika mashindano ya Olimpiki Rio de Janeiro mnamo Agosti.

5. Marufuku ya kutotoka nje

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viwanda vimelengwa katika maandamano Ethiopia

Huwezi kutembelea kiwanda, shamba au taasisi ya serikali kati ya saa kumi na mbili jioni hadi kumi na mbili alfajiri. Ukikiuka marufuku ya kutotoka nje, 'vikosi vya sheria vimeagizwa kuchukua hatua zipasazo'.

6. Wanadiplomasia

Haki miliki ya picha AFP

Kama wewe ni mwanadiplomasia hauruhusiwi kusafiri zaidi ya kilomita 40 kutoka mji mkuu Addis Ababa, bila ya ruhusa. Serikali inasema ni kwa usalama wako.

Kwa jumla hakujatolewa tamko lolote kidiplomasia kuhusu hali ya tahadhari ilioidhinishwa.

7. Bunduki

Kama unamiliki bunduki, huwezi kuibeba kufikia kilomita 25 za barabara kuu za mji mkuu Addis Ababa, na kufikia kilomita 50 za mipaka ya nchi hata kama una kibali cha umiliki.

Taarifa zaidi kuhusu maandamano ya Ethiopia