Al-Shabab lashambulia mji wa Afgoye Somalia

Vita vikali vinaendelea mjini Afgoye baada ya wapiganaji wa al-Shabab kushambulia mji huo Haki miliki ya picha AP
Image caption Vita vikali vinaendelea mjini Afgoye baada ya wapiganaji wa al-Shabab kushambulia mji huo

Wapiganaji wa kundi la al-Shabab nchini Somalia wameushambulia mji muhimu wa Afgoye,yapata kilomita 30 kutoka mji mkuu wa Mogadishu.

Kuna ripoti kuhusu mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari na mapigano makali,hususan karibu na afisi za serikali na kituo cha polisi.

Wakazi wameiambia BBC kwamba raia wengi pamoja na wanajeshi wamejeruhiwa.

Al-Shabab limesema kuwa wapiganaji wake wameuteka mji huo,lakini gavana wa jimbo hilo amesema kuwa wanajeshi wa serikali ya Somalia bado wanawakabili wapiganaji hao.

Mji wa Afgoye uko mkabala na barabara kuu inayounganisha Mogadishu na kusini mwa Magaharibi ya Somalia.