Kuahirishwa uchaguzi DRC 'huenda kukazusha ghasia'

Maandamano ya mwezi uliyopita yalikumbwa na ghasia na kusababisha watu 50 kuuawa. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano ya mwezi uliyopita yalikumbwa na ghasia na kusababisha watu 50 kuuawa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa ameshutumu uamuzi wa kuahirisha uchaguzi wa urais katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kutoka Novemba mwaka huu hadi 2018, shirika la habari la Reuters linaripoti.

Hatua hiyo iliidhinishwa na mahakama ya kikatiba nchini siku ya Jumatatu.

Wakosoaji wanatazama kuahirishwa kwa uchaguzi huo kama njia ya kuendelewa kumuweka rais Joseph Kabila madarakani - alitarajiwa kujiuzulu kufikia Desemba mwishoni mwa mwaka huu, wakati muhula wake wa pili unamalizika.

Tume ya uchaguzi inasema inahitaji muda zaidi kuiweka sawa orodha ya wapiga kura.

Reuters limemnukuu waziri wa mambo ya nje Ufaransa, Jean-Marc Ayrault anayesema:

"Kuna njia moja pekee kutoka katika mzozo huu, na hiyo ni kuwa Rais aitishe uchaguzi na asiwanie."

"Kuahirisha uchaguzi hadi katika tarehe isiyo ya hakika 2018 sio suluhu. Kuna hatari ya kuzuka maandamano ya fujo na ukandamizaji."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii