Marekani: IS inawatumia raia kama kinga Mosul Iraq

Baadhi ya wanajeshi wa Iraq mjini Mosul
Image caption Baadhi ya wanajeshi wa Iraq mjini Mosul

Wakati mapigano yakiendelea Iraq katika mji wa Mosul jeshi la Marekani linasema wapiganaji wa Islamic State wanawatumia raia kama kinga.

Msemaji wa ikulu ya marekani amesema kundi la IS limekuwa likiwazuia watu katika mji huo kinyume na matakwa yao.

Jeshi la anga la Marekani limekuwa likisaidia jeshi la Iraq na vikosi vingine vya usalama huku wanajeshi wao wakianza kuukaribia mji wa Mosul.

Lakini wakazi wa mji huo hawajahama kwa idadi inayotarajiwa.

Image caption Msikiti maarufu mjini Mosul uliojengwa karne ya 12

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu wamezitaka pande zote katika mapigano kuonyesha ubinadam kwa raia zaidi ya milioni moja wanaoishi Mosul.