Wakristo waadhimisha miaka 40 ya ibada za Kiswahili
Huwezi kusikiliza tena

Wakristo waadhimisha miaka 40 ya ibada za Kiswahili Uingereza

Jumuiya ya watu wanaouzungumza lugha ya Kiswahili hapa Uingereza, mwishoni mwa wiki iliyopita imefanya ibada ya shukran kuadhimisha miaka arobaini tangu kuanzishwa kwa ibada za Kikristo kwa lugha ya Kiswahili.

Maadhimisho yalihusisha watu wa madhehebu mbalimbali kutoka Afrika Mashariki na Kati. Kiswahili ni moja ya lugha rasmi barani Afrika na inakadiriwa, zaidi ya watu milioni mia moja na thelathini wanazungumza lugha hii duniani.

Zawadi Machibya alihudhuria maadhimisho hayo.