Pique: Man City wanacheza kama Barcelona

Gerrard Pique akiwa pamoja na aliyekuwa kocha wa Barcelona Pep Guardiola Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gerrard Pique akiwa pamoja na aliyekuwa kocha wa Barcelona Pep Guardiola

Klabu ya Manchester City imeanza kucheza mtindo wa Barcelona chini ya meneja wao Pep Guardiola,kulingana na beki wa timu hiyo ya La Liga Gerrard Pique.

Guardiola aliyewahi kuifunza Barcelona anarudi Nou Camp siku ya Jumatano huku kikosi chake kipya kikikabiliana na mabingwa hao wa La Liga.

Guradiola alishinda mataji 14 akiwa mkufunzi wa Barca kati ya 2008 na 2012,huku akifanya mtindo wao wa tiki-taka kuwa maarufu.

''Wanacheza kama sisi kwa sababu Pep alikuwa nasi hapa kwa miaka mingi''.

Kikosi cha Barcelona kilichokuwa kikifunzwa na Guardiola kilishinda michuano 14 kati ya 19 walioshiriki katika kipindi cha miaka 4 kama mkufunzi na akawa maarufu kwa mchezo wa pasi za kasi na ukabaji wa hali ya juu.

''Man City wanatoa presha ya juu kwa sababu wanapochukua mpira wanatafuta nafasi'' ,aliongezea Pique ambaye alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Barca wakati Guradiola alipochukua ukufunzi wa timu hiyo.

Anaelewa soka vile tunavyoielewa.Itakuwa mechi yenye changamoto nyingi''.