''Babangu alinidunga sindano yenye virusi vya Ukimwi''

Bryan Jackson miaka 24 baada ya kudungwa sindano yenye virusi vya ukimwi na babake Haki miliki ya picha BAILEY E KINNEY
Image caption Bryan Jackson miaka 24 baada ya kudungwa sindano yenye virusi vya ukimwi na babake

Wakati babaake Bryan Jackson alipomdunga sindano ya virusi vya HIV mwanawe mchanga,alitumai kwamba hatamuona akikuwa.

Hakuna mtu aliyedhani kwamba miaka 24 baadaye atakabiliana na mwanawe mahakamani ili kusikiliza athari za uhalifu alioufanya.

Wawili hao walikutana mahakamani licha ya kutoonana tangu Bryan alipokuwa mtoto.

Jackson yuko katika mahakama hiyo kusoma taarifa ambayo huenda ikamfunga jela babake kwa kipindi kirefu.

Ni taarifa ambayo watu wachache pekee waliamini angepata fursa ya kuisoma,wakati mwaka 1992 alipopatikana na ugonjwa wa ukimwi .

Yote haya yalianza wakati mamake na babake walipokutana katika kambi moja ya kijeshi mjini Missouri ambapo wote walikuwa wakijifunza utabibu.

Haki miliki ya picha FAMILIA YA JACKSON
Image caption Stewart Jackson na mwanawe Bryan kulia

Waliishi pamoja na miezi mitano baadaye kati kati ya mwaka 1991 mamake alishika mimba.

Wakati nilipozaliwa babangu alikuwa na furaha tele,lakini kila kitu kikabadilika alipoenda katika operesheni ya Desert Stom .

'Alirudi kutoka Saudia akiwa na tabia tofauti kunihusu',alisema Jackson.

Stewart alianza kukataa kwamba Jackson ni mwanawe,akitaka kufanyiwa ukaguzi wa vinasaba vya DNA na akaanza kumtusi mamake.

Wakati alipoachana na mamake,wazazi hao walikabiliana sana kuhusu mahitaji ya mtoto ,ambayo Stewart alikataa kulipa.Mara nyengine wakati wa vita vyao angemtishia mamake Jackson .

Alikuwa akitoa matamshi kama :Mwanao hataishi zaidi ya miaka mitano,na nitakapoachana nawe sitawacha chochote kinachotuunganisha.

Wakati huohuo Stewart ambaye alipata kazi kama mkaguzi wa damu katika maabara moja ,alianza kwa siri kuchukua violezi vya damu yenye maambukizi nyumbani,wachunguzi baadaye walibaini.

''Alikuwa akifanya utani na rafikize akisema:Iwapo ningetaka kumwambukiza mtu na virusi hivi ,wasingejua ni nini kilichowaathiri,alisema Jackson.

Wakati Jackson alipokuwa na miezi 11,mamake na babake walikuwa hawawasiliani,"lakini wakati Jackson alipolazwa kwa kuugua pumu'',mamake alishika simu.

Haki miliki ya picha FAMILIA YA JACKSON
Image caption Bryan na mamake

Mamaangu alimpigia simu kumuelezea,alidhani angetaka kujua iwapo mwanawe ni mgonjwa.

Alipopiga simu rafikize walishika simu na sema kuwa Bryan Stewart hana mtoto.

Siku ambayo Jackson alitolewa hospitalini,Stewart alimtembelea hospitalini.Na wakati matokeo yangu ya ukaguzi wa damu yalipotokea nilipatikana na ugonjwa wa Ukimwi.

Babangu alimtuma mamangu katika mkahawa mmoja ili kununua kinywaji ili aweze kubakia nami.

Alipoona hakuna mtu karibu,Stewart alichukua damu ilio na maambukizi ya ukimwi na kumdunga mwanawe.

''Alitumai ningefariki ili asilipe mahitaji ya mtoto'',alisema Jackson.