Mwana wa Ken Saro Wiwa afariki London

Mwana wa Ken Saro Wiwa Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Mwana wa Ken Saro Wiwa

Mwana wa mwanaharakati maarufu wa mazingira nchini Nigeria Ken Saro-Wiwa ambaye aliuawa miaka 20 iliopita amefariki mjini London.

Ken Saro Wiwa Jr mwenye umri wa miaka 47 alifariki baada ya kuugua kiarusi,kulingana na familia yake.

Alikuwa mwandishi aliyewahi kuwa mshauri wa marais watatu.

Mauji ya babake mwaka 1995 yaliotekelezwa na serikali ya kijeshi kwa kuongoza maandamano dhidi ya uharibifu wa mazingira yanayosababishwa na sekta ya mafuta yalizua hisia kali duniani.

Image caption Mwanaharakati wa mazingira nchini Nigeria marehemu Ken Saro Wiwa

Saro-Wiwa aliongoza vuguvugu la wakazi wa Ogoni ,ambalo lilishtumu shirika la mafuta la Shell kwa kuharibu mazingira nyumbani kwake katika jimbo la Ogoniland kusini mashariki mwa Nigeria.

Mauji yake baada ya kesi ya siri chini ya jenerali Sani Abacha yalisababisha Nigeria kuondolewa kwa muda miongoni mwa mataifa ya Jumuiya ya madola.