Aina mpya ya viazi vitamu kutoka Uganda
Huwezi kusikiliza tena

Aina mpya ya viazi vitamu kutoka Uganda

Mamilioni ya watoto duniani wanakabiliwa na tatizo la utapiamlo lakini aina mpya ya viazi vitamu ambavyo vinakuzwa na kustawishwa nchini Uganda inaweza ikawa suluhu.

Viazi vitamu hivyo, ambavyo ndani ni vya rangi ya machungwa vina viinilishe vya ziada kuliko viazi vitamu vya kawaida.

Viazi vitamu hivyo vinapata rangi hiyo kutokana na viinilishe vya beta-carotene, ambavyo ni muhimu katika kuupa mwili Vitamin A.

Mwandishi wa BBC Anne Kacungira anaarifu zaidi.