Wanawake kuandamana kupinga ubakaji

Waliombaka Lucia walimpa mihadarati Haki miliki ya picha FACEBOOK
Image caption Lucia Perez wa miaka 16 alibakwa hadi kufa

Maelfu ya wanawake nchini Arentina wameapa kususia kazi kulalamikia kifo cha msichana mmoja aliyebakwa hadi kufa. Lucia Perez mwanafunzi wa shule ya upili alibakwa mapema mwezi huu katika mji wa Mar del Plata.

Wanaume wawili walimpeleka hospitalini na kusema alikua ametumia mihadarati kupita kiasi. hata hivyo madaktari walimchunguza na kupata alikua amebakwa na kuharibiwa vibaya.Wanawake wote wanaandamana katika mji mkuu, Buenos Aires na wakia na mavazi meusi.

Wanaharakati wameomba wanawake wote kuondoka afisini, viwandamani, nyumbani, shule na hata waandishi wa habari wa kike na kuandamana kupinga ukatili huo. Kumekuwepo na maandamano nchini Argentina kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kulalamikia dhuluma dhidi ya wanawake.

Image caption Ubakaji ulifanyika eneo la Mar del Plata

Nchi hiyo iliidhinisha sheria dhidi ya mauaji ya wanawake na kuwema adhabu kali kwa wanaopatikana na makosa ya kuwaua wanawake kwa sababu za ubaguzi wa kijinsia. Pia sheria hiyo inaangazia vita vya nyumbani. Wanaume watatu wamekamatwa kutokana na kifo cha Lucia.

Wakuu wa mashtaka wamesema msichana huyo alipewa bangi na dawa za kulevya aina ya Cocaine, kabla ya kubakwa. Watesi wake wakimsababisha uchungu kiasi cha marehemu kupatwa na mshutuko wa moyo.Alifariki punde baada ya kufikishwa hospitalini.