Mapigano kusitishwa kwa siku tatu Yemen

Mapigano hayo ni baina ya vikosi vya serikali na waasi wa Houthi katika picha
Image caption Mapigano hayo ni baina ya vikosi vya serikali na waasi wa Houthi katika picha

Mpango wa kusitisha mapigano kwa siku tatu unakaribia kuanza nchini Yemen.

Upande wa serikali ambao unaungwa mkono na Saudi Arabia na waasi wa Houth wamekubaliana na umoja wa mataifa kusitisha mapigano.

Kunaripoti zisemazo kuwa mapigano makali yanaendelea mpaka kufikia kusitisha mapigano, na kuna tetesi kwamba yatasitishwa.

Lakini umoja wa mataifa unatumaini kuwa kusitisha mapigano kunaweza kupelekea kuendelea kwa mazungumzo ya amani.

Image caption Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, takriban watu 7,000 wameuawa katika mapigano hayo

Kwa zaidi ya miezi minane ya vita ya wenyewe kwa wenyewe kumeleta hali ngumu ya maisha kwa raia nchini Yemen.

Kwa sasa zaidi ya watoto milioni moja wanabiliwa na utapiamlo kwa kiwango cha juu.