Waandamana Argentina kupinga ubakaji wanawake

Msichana aliyeuawa kwa kubakwa Argentina Haki miliki ya picha facebook
Image caption Msichana aliyeuawa kwa kubakwa Argentina

Maelfu ya watu nchini Argentina wameshiriki maandamano dhidi ya tukio la kutisha la kubakwa na kuuawa kwa msichana mwezi uliopita.

Lucia Perez, aliyekuwa na umri wa miaka 16, alilishwa dawa za kulevya na kubakwa kabla ya kuuawa katika mji wa pwani wa Mar del Plata.

Maelfu ya waandamanaji waliovalia nguo nyeusi waliandamana mjini Buenos Aires na mingine ya Argentina.

Wengi wanataka kuchukuliwa kwa hatua kali dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia.

Nchini Argentina mwanamke mmoja anauawa kila baada ya saa 36, sababu ikiwa ni udhalilishaji wa kijinsia.