Uefa: Barcelona yaiua Manchester City ya kocha wake wa zamani

Messi amefunga magoli 10 katika michezo nane ya mwisho ya ligi ya mabingwa Ulaya
Image caption Messi amefunga magoli 10 katika michezo nane ya mwisho ya ligi ya mabingwa Ulaya

Michuano ya klabu bingwa ulaya imeendelea kwa michezo nane kupigwa ambapo Arsenal waliiadhibu Ludogorets Razgrad ya Bulgaria 6-0, wakati Mesut Ozil akipata hat trick.

Barcelona nayo wakiwa nyumbani walimdhalilisha kocha wao wa zamani Pep Guardiola kwa kumpa kichapo cha 4-0, Messi nae akipiga hat-trick, ambapo katika mchezo huo ilishuhudiwa mlinzi wa Man city Claudio Bravo akilambwa kadi nyekundu huku pia mlinzi wa Barcelona aliyeingia akitokea benchi Jeremy Mathieu naye akizawadiwa kadi nyekundu.

Image caption Bravo atakosa mchezo wa maruduiano Novemba 1

Makosa ya wazi ya mlinzi wa Celtic Kolo Toure yakaipa Borussia Monchengladbach ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini, magoli yakifungwa na Lars Stindl pamoja na Andre Hahn.

Image caption Wachezaji wa Arsenal wakifurahia ushindi mnono

Matokeo ya michezo mingine

Bayern Munich 4-1 PSV Eindhoven

Paris Saint-Germain 3-0 Basel

Dynamo Kiev 0-2 Benfica

Napoli 2-3 Besiktas

FC Rostov 0-1 Atl├ętico Madrid