Mdahalo Marekani: Mshindi ni nani - Trump au Clinton?

Trump na Clintone kwenye TV Haki miliki ya picha Getty Images

Huenda huu ulikuwa mjadala alio utaka Donald Trump, lakini haukuwa mjadala anao uhitaji.

Akiwa na nafasi ya mwisho kuuvutia umma wa Marekani kwa kuwaeleza ni kwanini anapaswa kuaminiwa kuwa rais wa Marekani , mgombea huo wa Republican alilazimika kung'ang'ana kutafuta uungwaji mkono.

Alilazimika kutafuta njia kujitenga na tuhuma kuwa alikuwa na historia ya unyanyasaji wa kingono.

Ilibidi ajitokeze kama mgombea atakayeleta mageuzi - siku kadhaa baada ya kura ya kutafuta maoni ya kituo cha televisheni cha Fox kudhihirisha kuwa Hillary Clinton, ambaye chama chake kimeshikilia urais kwa miaka 8, anamshinda katika suala la, 'ni nani atakaye igueza nchi kuwa bora zaidi'.

Badala yake, baada ya nusu saa ya kilicho onekana kuwa mjadala wa sera kuhusu mahakama ya juu zaidi nchini, haki za kumiliki bunduki, uavyaji mimba na pia suala la uhamiaji, Donald Trump kama alivyozoeleka - alianza kumkatiza mpinzani wake, alianza kujibizana na muendesha mjadala na kuwakemea maadui zake wa kweli na anaowadhania.

Alimuita Bi Clinton 'muongo na mwanamke muovu'.

Amesema wanawake wanaomshutumu kuwanyanyasa kingono, aidha ni watu wanaotaka kujulikana au wafuasi wa kampeni ya Clinton.

Na Clinton naye alilazimika kwa wakati wake kujitetea kuhusu barua pepe zake, wakfu wa familia yake Clinton na taarifa za aibu zilizofichuliwa katika mtandao wa Wikileaks.

Haki miliki ya picha AP

Tofuati hatahivyo, ni kuwa Bi Clinton kwa ukubwa alimakinika, na kufanikiwa kukwepa maswali na badala yake kugeukia mengine ambayo hakuwa na tatizo kuyajibu.

Jambo kubwa lililojitokeza katika mjadala huu hatahivyo - kichwa kikuu watakacho kienukia raia Marekani asubuhi - ni hatua ya Trump kukataa kuachana na madaia yake ya kuwepo 'udanganyifu' katika uchaguzi ujao.

Hilo ndilo jambo alilotaka kusema Trump, lakini sio jambo ambalo raia wa Marekani au demokrasia ya taifa hilo ilihitaji kusikia.

'Kinyago cha Urusi'

Kwa wakati mmoja Bi Clinton alijaribu kugeukia suala la iwapo Trump atakana kuitambua serikali ya Urusi ambayo maafisa Marekani wanasema ndiyo inayohusika na uvamizi wa mtandao.

Trump amesema hajaonana na Putin (licha ya kujigamba katika mjadala wa chama chake kuwa alizungumza naye katika chumba kimoja cha televisheni), na kusema kuwa Bi Clinton ni muongo na ndiye 'kinyago' cha kweli kinachoendeshwa na Urusi.

Wakati mbaya

Wakati wa kitengo cha kujadili uchumi, baada ya majadiliano kuhusu ulipaji kodi wa kila mgombea, na majibizano kuhusu nani anayepunguza au kuongeza kodi zaidi ya mwenziwe, Trump alimkabili Clinton kuhusu makubaliano yake ya kibiashara ya siku za nyuma.

Haki miliki ya picha AFP

Clinton alipojiuma kidogo, Trump alijaribu kutumia kauli aliyotumia katika mjadala wa nyuma na kwa ufanisi.

Ni kwanini Clinton hakuidhinisha mageuzi anayopendekeza sasa miaka 30 ya nyuma alipokuwa akiitumikia serikali? Trump aliuliza.

"Ulihusika na kila suala la nchi hii," alisema. "Na una uzoefu, hilo ndio jambo unalo nizidi nalo, lakini ni uzoefu mbaya, kwasababu ulichokifanya mpaka sasa kimegeuka kuwa kibaya."

Tatizo la kuregelea kauli ya kumshambulia mtu ni kuwa huenda mpinzani amejitayarisha na jibu, na Clinton alikuwa tayari kumjibu kwa hilo.

Alisema wakati akitetea haki za watoto miaka ya 70, Trump alikuwa anajitetea katika kuwanyanyasa raia weusi wa Marekani katika mradi wa nyumba.

Wakati Clinton alipokuwa anatetea haki za wanawake miaka ya 90, Trump alikuwa anamkejeli mshindi wa maonyesho ya urembo kuhusu uzito wa mwili wake.

Na wakati alikuwa ikulu ya White House akitazama shambulio dhidi ya Osama bin Laden, Trump alikuwa anaendesha kipindi kwenye tv.

Tuhuma za udanganyifu

Trump alikuwa tayari kesha didimia katika mjadala wakati huu.

Bi Clinton alifanikiwa kukwepa anavyomshambulia na kumchochea kuitokeza tabia iliyompunguzia umaarufu baada ya mjadala wa kwanza.

Alihitaji ushindi wa wazi, na kwa kiwango fulani alikuwa katika kiwango sawa na Clinton.

Alafu akaulizwa kuwa licha ya kauli aliyoitoa kwenye mkutano wake wa kisiasa kuhusu kuwepo udanganyifu wa kura, je anaweza kufuata mfano wa mpinzani wake na aahidi kukubali matokeo ya kura?

"Nitaliangalia wakati huo," alisema. "Siangalii chochote kwa sasa."

Haki miliki ya picha Reuters

Ni kauli itakayosalia kwenye vichwa vya habari na kugubika majadiliano katika siku zijazo.

Jibu la Clinton ni kuwa kauli hiyo ya mgombea wa Republican ni ya "kutisha".

Katika kuzungumza na maafisa wa Republican baada ya mjadala, ilionekana wazi wasi wasi wao kuzungumzia kauli yake Trump.

Baadhi walisema ni mzaha tu.

Wengine wakasema ni kuwa Trump hataki kufikiria kushindwa kabla ya siku ya uchaguzi.

Hatahivyo ukweli ni kuwa, viti walivyopata wanachama wa Republican vya sasa, vya siku za nyuma na hata siku zijazo, ni kutokana na kura za raia, na wanategemea ukweli unaotokana na wapinzani wanaokubali wakati wakishindwa.

Trump ametilia shaka demokrasia Marekani . Na anapoutikisa mti huo, ni vigumu kubaini ni nani atakayeumia kwa matawi yanayoanguka.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii