Mbwa azikwa hai akiwa amedungwa msumari kichwani

Mbwa azikwa akiwa hai huku akiwa amedungwa msumari kichwani
Image caption Mbwa azikwa akiwa hai huku akiwa amedungwa msumari kichwani

Mbwa mmoja amepatikana amezikwa akiwa hai huku msumari ukiwa umedungwa kichwani mwake katika eneo la Teesside katika kile shirika linalokabiliana na unyanyasaji wa wanyama nchini Uingereza RSPCA linasema ni kitendo cha ukatili.

Wanandoa wawili waliokuwa wakitembea katika eneo la Kirkleatham Wood ,walisikia kilio cha kitu kilichokuwa kikilia kwa uchungu na kumpata mbwa huyo ambaye tayari alikuwa amezikwa.

Alikimbizwa kwa daktari wa wanyama lakini majeraha yake mabaya yalimlazimu mtabibu huyo kumuua.

Shirika hilo la wanyama linasema kuwa zaidi ya mtu mmoja alihusika katika kitendo hicho.

Inspekta Nick Jones alisema: katika kipindi cha miaka kumi ambacho nimefanyia kazi RSPCA,sijawahi kuona kitu cha kuogofya na ukatili mkubwa kama huu.