Mjadala wa 3 wa urais kati ya Trump na Clinton

Mjadala wa tatu wa urais kati ya Clinton na Trump
Image caption Mjadala wa tatu wa urais kati ya Clinton na Trump

Madai: Donald Trump anasema kuwa ghasia katika baadhi ya mikutano yake ikiwemo ule wa Chicago zilisababishwa na kampeni ya mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton na rais Barrack Obama.

Ukweli:Hii inahusishwa na kanda za video zilizotolewa na mradi wa mwanablogu wa mrengo wa kulia James O'Keefe.

Kanda za kamera zilizofichwa zinaonekana zikionyesha kampuni zinazounga mkono kampeni ya Hillary Clinton pamoja na kamati ya kitaifa ya chama cha Democrat zikizungumza kuhusu kuwafunza watu waliojitolea kuhudhuria mikutano ya Trump na kuzua ghasia.

Mmoja wao ,Scott Foval,anasikika akisema haikuchukua muda mwingi kuchochea ghasia miongoni mwa mashabiki wa Trump kwa sababu wana matatizo ya kiakili.

Wengine wanaonyeshwa wakijigamba kuzua fujo nje ya mkutano wa Trump mjini Chicago.

Foval alifutwa kazi kama mkurugenzi wa kitaifa wa maswala ya mashinani katika kampeni ya Clinton siku ya Jumatatu kutokana na kanda hizo.

Robert Creamer mwanakandarasi mwengine wa Democrat ambaye alihusika katika mpango huo wa hila chafu,madai,licha ya kusema kuwa mazungumzo kama hayo hayakufanyika.

Kampeni ya Clinton imekana kuwaweka waandamanaji na kuzua ghasia kwa makusudi katika mikutano ya Trump.

Huku mradi huo ukidaiwa kutoa kanda ya video isio sahihi,baadhi ya mbinu zilizotumika katika video hiyo zina tatiza licha ya mpango huo kutofanyika,alisema Zac Petkanas,msemaji wa kampeni ya Clinton katika taarifa yake.

''Tunaunga mkono hatua ya kamati ya kitaifa ya Democrat katika kutatua swala hili na tutaendelea kufanya kampeni yenye mawazo endelevu''

Lakini shabiki wa Trump Jeffrey Lord aliambia CNN kwamba mrengo wa kushoto wa Marekani una tabia kama hizo na hilo halikubaliki kabisa.

Image caption Donald Trump

Trump amekuwa akisema mara kwa mara kwamba rais wa Urusi Vladimnir Putin amekuwa akimsifu.

Ukweli:Hili halionekani kuwa ukweli.

Mwaka 2015,Putin alitumia neno 'Yarkii' kumtaja mgombea huyo wa Republican kuwa mwerevu.

Putin mwenyewe ,alikana neno ''kipaji'' mnamo mwezi Juni katika mahojiano na CNN.

''Ulitoa matamshi fulani kuhusu mgombea wa urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump''.ulimtaja kuwa bora na mwenye ''kipaji', mwandishi wa CNN fareed zakaria alisema.

Matamshi hayo yaliripotiwa dunia nzima.

''Nilikuwa nataka kujua ni nini kilichokuvutia kutoa uamuzi huo, na je bado unashikilia msimamo huo''? ''Kwa nini kila mara unabadilisha ninachokisema''? Putin alijibu kupitia mkalimani.

''Nilisema pekee kwamba ni mwerevu,wadhani si mwerevu''?,ndiye.Sikusema lolote jingine kumhusu''.

Hillary Clinton naye anatetea uamuzi wake wa sheria ya kudhibti bunduki nchini humo kwa kusema kuwa nchini Marekani kuna vifo takriban 33,000 vinavyosababishwa na bunduki kila mwaka.

Ukweli: Takwimu za Clinton zinatoka katika kituo cha kudhibiti magonjwa na uzuiaji wa vifo.Takwimu hizo ni za mwaka 2014,ambazo ni za hivi karibuni kutolewa.

Ili kusawazisha asilimia 33 ya vifo vya mauaji,asilimia 63 ikiwa ni watu wanaojiua.

Donald Trump mara kwa mara amekuwa akitumia Chicago kama mji ambao una visa vingi vya ghasia ambazo haziwezi kudhibitiwa.

Ukweli:Viwango vya mauji ya Chicago viko juu zaidi ikilinganishwa na miji mingine kama vile New York na Los Angeles.

Kufikia sasa mwaka huu zaidi ya watu 600 wameuawa,ikiwa ni ongezeko la asilimia 24 ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka uliopita.

Trump amekuwa akidai kwa siku kadhaa sasa kwamba mfumo wa upigaji kura umefanyiwa udanganyifu mbali na kukabiliwa na maswala ya ufisadi,na kwamba udanganyifu miongoni mwa wapiga kura ni jambo la kawaida.

Ukweli:Trump ananukuu kutoka kwa utafiti wa mwaka 2012 uliofanywa na shirika moja lisilopendelea upande wowote Pew, ambalo linakadiria kwamba takriban watu milioni 24 ama mmoja kati ya kila wanane sio halali tena na kwamba kuna makosa.

Kati yao,ripoti hiyo inasema ,wapiga kura milioni 1.8 walifariki.

Lakini ripoti hiyo ya Pew, haisema kwamba watu miloni 1.8 waliofariki walishiriki katika upigaji kura.

Ilisema kuwa makosa yaliopo ni ushahidi wa kuimarisha mfumo wa usajili wa wapiga kura.

Watafiti wengine wanasema kuwa udangayifu katika upigaji kura unaohusisha masunduku ya kupiga kura kuhusu kura zilizopigwa na watu waliofariki ni jambo lisilo la kawaida.

UKweli: George W Bush alipunguza kodi miongoni mwa watu wanopokea mapato ya hali ya juu kutoka asilimia 39.6 hadi 35.

Chini ya mpango wa Trump,kodi ya watu wanaopata mapato ya juu itapunguzwa kutoka asilimia 39.6 hadi 33.

Trump anamshambulia Clinton kuhusu rekodi yake ya kuwa mamlakani,akimwambia: Wakati ulipokuwa waziri wa maswala ya kigeni ,takriban dola milioni 6 zilitoweka ,pengine ziliibwa....hakuna anayejua.

Ukweli:Ni madai ambayo yametolewa na Trump hapo awali ..na madai ambayo yamethibitishwa kuwa ya uongo.

Donald Trump anadai kwamba Bi Clinton anaunga mkono uavyaji mimba ,akidai unaweza kufanyika siku mbili au tatu kabla ya mtoto kuzaliwa.

Ukweli:Hii inatokana na matamshi yaliotolewa na Clinton wakati wa kampeni za chama cha Demokratic aliposema kuwa uavyaji wa mimba kubwa unatokana na ''mahitaji ya kimatibabu''.

Alimwambia Trump wakati wa mjadala: Hicho sio kinachofanyika wakati huo.Na anasema ukweli-kwamba uavyaji wa mimba kubwa unaotajwa na Trump una visa vichache sana.

Data iliopatikana kutoka kwa taasis ya Guttmacher inaonyesha kwamba uavyaji mimba mwingi hufanyika mapema.

Image caption Hillary Clinton

Ni aslimia 1.2 ya visa vya uavyaji mimba nchini Marekani, ambavyo ni 12,000 kwa mwaka,hutokea baada ya wiki 21.

Baadhi ya majimbo 43 tayari yanapinga uavyaji mimba katika kiwango fulani ,kwa hivyo uavyaji wa mimba kubwa umepigwa marufuku katika maeneo mengi ya taifa hilo.