Meya awasuka nywele wanawake kuvutia kura Ghana

Meya wa Accra Ghana awasuka nyewel wanawake kuvutia wapiga kura Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Meya wa Accra Ghana awasuka nywele wanawake kuvutia wapiga kura

Huku ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa bunge na urais nchini Ghana,wagombea wanatumia kila njia ili kuwavutia wapiga kura.

Wengi hugawanya nguo,chakula na fedha kwa lengo la kuwavutia wapiga kura.

Hatahivyo ,meya wa mji mkuu wa Accra, Alfred Oko Vanderpuije,ametumia njia tofauti zaidi ili kuweza kuhifadhi kiti chake.

Mapema wiki hii, picha zilionekana katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha Meya huyo kwa jina maarufu Tsentse,akiwasuka nywele wanawake pamoja na kupika chakula kinachopendwa na wengi cha mchanganyiko wa muhogo na mahindi.