Yemen: Waasi washutumiwa kwa kuvunja makubaliano ya amani

Kusitishwa kwa mapigano kutapelekea mazungumzo ya amani
Image caption Kusitishwa kwa mapigano kutapelekea mazungumzo ya amani

Muungano wa jeshi linaloongozwa na Saudi Arabia amabalo linaunga mkono upande wa serikali ya Yemen umewashutumu waasi kwa kuvunja makubaliano mara kwa mara ya kusitisha mapigano.

Muungano huo unasema kuwa waasi wa Houthi wameshavunja makubaliano zaidi ya mara arobaini pembezoni mwa mpaka wa Saudi Arabia.

Wakati huohuo waasi wa Houthi wamesema shambulizi la anga katika eneo lao limewauwa raia watatu.

Umoja wa Mataifa ulitumai kuwa usitishwaji wa mapigano ungeongezwa ili kupisha mazungumzo ya Amani.