Theresa May ahudhuria mkutano wa kwanza wa umoja wa Ulaya

Theresa May amealikwa kwenye mkutano huo kutoa muelekeo wa nchi yake juu ya siku haswa ya kujitoa kamili
Image caption Theresa May amealikwa kwenye mkutano huo kutoa muelekeo wa nchi yake juu ya siku haswa ya kujitoa kamili

Waziri mkuu wa Uingereza,Theresa May, yupo mjini Brusels nchini Ubelgiji kwa mkutano wake wa kwanza wa Umoja wa Ulaya tangu kuingia madarakani katika kura ya Uingereza kujitenga na Muungano wa Ulaya.

Amesema atawaambia wenzake kwamba Uingereza itatoa mchango wake kikamilifu hadi kuondoka kwake, na utakuwa imara na wenye kutegemea washirika baadae.

Lakini Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ameonya kuwa kama Bi May alitaka kujiondoa kikamilifu katika Umoja wa ulaya, kungekuwa vigumu kukubaliana katika miezi ya mbeleni.

Taarifa zinasema serikali ya Bi May ina mgawanyiko juu ya biashara gani Uingereza inapaswa kulenga.

Uingereza inatarajiwa kuanza mchakato wa kujiondoa rasmi mwishoni mwa mwezi Machi mwaka ujao.