Sababu ya Mfalme wa Morocco kuzuru Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Sababu ya Mfalme wa Morocco kuzuru Tanzania

Kwa mara ya kwanza, Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, Jumapili hii anaitembelea Tanzania kwa ziara ya kikazi baada ya kuzuru Rwanda.

Miongoni mwa ajenda kuu za ziara yake ni kuishawishi Tanzania kuiunga mkono Morocco kurejeshwa katika Umoja wa nchi za Afrika. Aidha, atatia saini mikataba ya kibiashara na kidiplomasia kati ya Tanzania na Morocco.

Mfalme Mohammed VI pia atazuru pia Ethiopia.

Mwandishi wetu wa Dar es Salaam Arnold Kayanda amezungumza na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga na kuandaa taarifa hii.