Nini kitafanyika Trump akikataa matokeo ya uchaguzi

Trump

Chanzo cha picha, Getty Images

Mgombea wa Republican Donald Trump ameashiria kwamba huedna akapinga matokeo ya uchaguzi wa urais iwapo atashindwa.

Matamshi yake yaliungwa mkono na wafuasi wa kampeni yake, lakini yanakiuka utamaduni wa muda mrefu katika siasa za Marekani kuwa mshindwa anatambua matokeo na kumpongeza mpinzani wake.

Hili limelinganishwa na hali ilivyokuwa wakati matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2000 wakati George W Bush alipomshinda Al Gore.

Nini kilichofanyika?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wagombea urais mwaka 2000 George W Bush na Al Gore

Kinyanganyiro kati ya Bwana Gore, mgombea wa Democrat, na yule wa Republican George W Bush mnamo 2000 ni mojawapo ya ushindani wa karibu zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Matokeo yalishikana katika jimbo la Florida, ambako tofuati ndogo ya ushindi ilisababisha kesi nyingi na mvutano wa kisheria wa wiki kadhaa jambo lililosababisha kura kuhesabiwa upya.

Mvutano huo ulifika katika mahakama ya juu zaidi, ambayo ilisitisha kuhesabiwa upya kura hizo.

Bush alipewa ushindni kwa kukabidhiwa kura zilizokuwa zinapingwa.

Gore, aliyeshinda kura za umaarufu kwa tofuati ya zaidi ya kura laki tano lakini alishindwa kwa tofuati ndogo Florida, hatimaye alikubali kushindwa Desemba 13 mwaka 2000.

Kwa hivyo Trump anaweza kufanya nini?

Trump ananafasi ndogo ya kufanya maamuzi. Kama iivyokuwa kwa Al Gore, iwapo matokeo yatakuwa na tofuati ndogo atakuwa na haki kisheria kupinga matokeo na kuitisha kura zihesabiwe upya.

Iwapo anaamini kuwa kuna udanganyifu umefanyika katika uchaguzi , anaweza kuwasilisha kesi dhidi ya maafisa katika majimbo yoyote anayoshuku kuwa wamehusika.

Katika hali ambapo Bi Clinton atashinda kwa uiwngi mkubwa, Trump anaweza kukataa kukubali kushindwa lakini hakuna anachoweza kufanya kubadili matokeo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini wakati kutakataa kwake kukubali matokeo hakuwezi kubadili hali, hatua hiyo itatizamwa kama pigo kwa mfumo wa demokrasia na siasa Marekani.

Lakini kukataa matokeo kunaweza kuzusha matatizo

Iwapo Trump atashindwa na akatae kukubali kushindwa, huenda athari ikapita kiwango cha kwenda mahakamani.

Tuhuma zake za kuwepo udanganyfu katika uchaguzi zikichanganywa na hatua yake kukataa kushindwa, kunatishia ghasia kuzuka miongoni mwa wafuasi wake.

Tajiri huyo wa chama cha Republican ana wafuasi wengi wa karibu na wengi wao wanaamini na mtu wa kando anayelengwa na wasomi wa kisiasa wa Washington.