Trump na Clinton wapambana tena katika mdahalo

wagombea Urais Marekani katika mdahalo Haki miliki ya picha AFP
Image caption wagombea Urais Marekani katika mdahalo

Wagombea Urais nchini Marekani Donald Trump na Hilary Clinton wamechuana tena katika awamu ya tatu na ya mwisho ya mdahalo mjini Las Vegas, ikiwa zimebaki siku chache tu, kabla ya kufanyika uchaguzi nchini humo.

Wamepambana vikali katika masuala mbalimbali ikiwemo umiliki wa silaha, utoaji mimba na uhamiaji haramu.

Na moja kati ya eneo waliovutana ni kuhusu uhusiano kati Marekani na Urusi na silaha za nyuklia.

Wakati Donald Trump akionyesha kuna haja ya uhusiano na Urusi na rais Vladmir Putin, Hillary Clinton anaona Urusi ni hatari kwa Marekani na hata kutupiana maneno makali.

Kuhusu umiliki wa silaha mgombea urais wa Democratic amesisitizia msimamo wake kuhusu sheria kali katika umiliki wa silaha.

Kwa upande wake Donald Trump alimshutumu Bi Clinton kwamba amejinufaisha kwa fedha zisizo halali.