UN: Mustakabali wa maisha mijini

Wakati miji inaendelea kupanuka, ukuwaji mwingi haukupangwa wala kukaguliwa (Colombia)

Chanzo cha picha, UN Habitat

Maelezo ya picha,

Wakati miji inaendelea kupanuka, ukuwaji mwingi haukupangwa wala kukaguliwa

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa miji 'kufanya maamuzi magumu' ili kuhakikisha miji salama na endelevu katika miaka ijayo.

Ban aliyasema hayo katika hotuba liotoa kwenye kikao cha tatu cha Shirika la Umoja wa mataifa kuhusu makaazi kinachofanyika mara moja kila baada ya miaka 20.

Maeneo mengi ya mijini ambako kuna zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani wanaoishi huko, yanaendelea kujengwa bila mpangilio wala ukaguzi, wataalamu wanaonya.

Chanzo cha picha, UN Habitat

Maelezo ya picha,

Usafiri wa ni tatizo katika maeneo mengi ya mjini

"Meya wa miji ndio walio katika mstari wa mbele katika vita vya kuidhinisha maendeleo," Ban ameuambia umati katika mkutano wa kimataifa wa ma Meya, ulioandaliwa katika kikao hicho cha tatu cha Umoja wa mataifa.

Lakini ameongeza pia ni lazima "wafanya maamuzi magumu kuhusu kipi kilicho muhimu" kwasababu ni lazima wawajibike kwa bajeti ndogo walizo nazo.

Ban amewaambia viongozi hao wa miji na wanaisasa kwamba wao ndio wakuu katika kuidhinisha makubaliano ya kimataifa, kama vile malengo endelevu ya maendeleo ya Umoja wa mataifa na makubaliano ya Paris ya mabadiliko ya hali ya hewa.

"Ni lazima muongoze ajenda hii muhimu - Muwatetee watu munao wawakilisha," aliwaomba.

'Ajenda iliyo sahaulika'

Kikao hicho ambacho Umoja wa mataifa umekitaja kuwa mojawapo ya vikao vikubwa katika historia ya Umoja huo, kimelenga kuidhinisha maazimio yatakayosaidia kupanga na kuidhinisha maendeleo katika miji katika miaka 20 ijayo.

Agenda hiyo mpya ya miji inatambua kuwa ukuwaji wa miji ni suala muhimu katika maendeleo kwenye karne ya 21, ameeleza Joan Clos, mkurugenzi mtendaji na katibu mkuu wa kikao hicho cha UN Habitat.

Ameeleza kuwa matukio ya hivi karibuni , kama mzozo wa fedha duniani na mapnduzi ya mijini kama wakati wa mapinduzi katika nchi za kiarabu, yamedhihirisha umuhimu wa maendeleo endelevu mijini.

Chanzo cha picha, UN Habitat

Maelezo ya picha,

Wakati miji inaendelea kukuwa na kuvutia mamilioni ya wahamiaji wa ndani kila mwaka, sekta isiyo ya kibinafsi ndio chanzo cha uchumi kwa wengi

Enzi ya karne ya 20

Kikao cha Habitat III kilijulikana kama Kikao cha Umoja wa matiafa kuhusu makaazi na maendeleio endelevu ya mijini .

Ni kikao cha tatu katika msururu wa vikao vya kimataifa vinavyofanyika mara moja kila baada ya miaka 20.

Kikao cha kwanza kilifanyika Vancouver, Canada mnamo 1976, na cha pili kiliandaliwa Istanbul, Uturuki, mnamo 1996.

Wakati huo idadi ya watu duniani imegeuka kutoka wakaazi wa vijiji na kuwa wakaazi wa miji huku asilimia 54 ya watu wakiwa sasa wanaishi katika maeneo ya mijini.

Utabiri unaashiria kuwa aislimia hiyo inatarajiwa kufika 66 kufikia katikati mwa karne hii.