Vikosi vya usalama Iraq vinasema vimeudhibiti mji wa Kirkuk

Vikosi vya Kikurdi vilijumuika na wanajeshi wa Iraq katika operesheni hiyo Haki miliki ya picha Reuters

Vikosi vya serikali ya Iraq vinasema kwamba vimedhibiti kamilifu mji wa Kirkuk, ambao ulivamiwa na wapiganaji wa Islamic state ijumaa.

Marufuku ya kutoka nje iliyowekwa sasa imeondolewa.

Chifu wa mji huo Khattab Omar Aref ameambi wanahabari kwamba wapiganaji wote 48 wamuwawa ama wamejilipua wakati wa makabiliano.

Afisa mkuu wa Pentagon amesema kwamba Washington imefurahishwa na operesheni hiyo ikizingatiwa ugumu wa oparesheni yenyewe.

Haya yanajiri huku Vita vikali vya kuwafurusha wapiganaji wa Islamic state kutoka kwenye mji wa kaskazini mwa Iraq Mosul, vikiiingia siku ya sita, huku vikosi vya Iraq vikikumbana na upinzani mkali.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vikosi vya Kikurdi vilijumuika na wanajeshi wa Iraq katika operesheni hiyo

Mwandishi wa BBC anayeandamana na wanajeshi wa Syria anasema kwamba wapiganaji hao wanatumia washambulizi wakujitolea kufa, kwa kutumia magari yaliyojazwa vilipuzi, na kuendeshwa kwa kasi kwenye maeneo ya vikosi vya serikali.

Vikosi vya serikali vinatumia makombora ya kushambulia vifaru.

Wapiganaji wa kikurdi pia wanakumbana na upinzani mkali katika eneo la Ba'ashiqah.

Kuna hofu kwamba zaidi ya raia milioni moja huenda wakakwama mjini Mosul.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii