Bunge lapiga marufuku uuzaji na utengezaji pombe Iraq

Pombe ni marufuku nchini Iraq
Image caption Pombe ni marufuku nchini Iraq

Bunge nchini Iraq limepiga kura ya kupiga maraufujku uuzaji na utengenezaji wa pombe.

Wanaounga mkono walisema kuwa hatua hiyo inatokana na tekelezwaji wa sheria yoyote inayoenda kinyume na Uislamu.

Hatahivyo wanaopinga wanasema kuwa sheria hiyo inakiuka uhuru wa kuabudu pamoja na kukandamiza makundi madogo kama vile yale ya dini ya Kikristo.

Wamesema kuwa wantaka rufaa mahakamani.

Afisa mmoja ameambia chombo cha habari cha AFP kwamba marufuku hiyo iliwekwa katika sheria ya mabaraza.

Sheria hiyo imepitishwa wakati ambapo serikali iko katika harakati za kuukomboa mji wa Mosul kutoka kwa kundi la wapiganaji la Islamic State.