Teknolojia kuboresha huduma ya afya
Huwezi kusikiliza tena

Teknolojia kuboresha huduma ya afya nchini Tanzania

Je ,umewahi kupata madhara yeyote baada ya kumeza au kupaka dawa au hata kudungwa sindano ? Kama jibu lako ni ndio ,je uliweza kutoa taarifa ili upate msaada?

Sasa Kutokana na ukuaji wa teknolojia ,Mamlaka ya udhibiti dawa na chakula nchini Tanzania(TFDA) imeanzisha mfumo maalum wa kielectronic utakaomwezesha mtumiaji wa dawa yeyote kuweza kutoa taarifa pale anapokutana na madhara yeyote ili iweze kufika sehemu husika,

Ili kufahamu zaidi, Mwandishi wetu Esther Namuhisa alizungumza na mmoja wa waanzilishi wa mfumo huo ambae pia ni mtaalamu wa tiba na dawa -Dr.Sajjad Fazel