Je wajua kuna ugonjwa wa mzio wa maji?

Mtu aliyeathiriwa na mzio wa maji
Image caption Mtu aliyeathiriwa na mzio wa maji

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa visa vya watu wenye mzio wa maji ni vichache.

Kampeni dhidi ya mzio ,shirika la hisani la kukabiliana na mzio linasema kuwa kuna visa 35 vinavyojulikana duniani.

Kwa sababu hiyo,uwezo wa wanasayansi katika kuutambua ugonjwa huo ni mdogo mno.

Ukijulikana kwa jina Aquagenic Urticaria,ni ugonjwa ambao hata wataalam wa matibabu hawaujui.

Ugonjwa huo husababisha vipele vidogo vidogo mwilini.

Lakini baada ya kujadiliana kuhusu hali hiyo katika BBC radio 2 kipindi cha Jeremy Vine,kundi la utengenezaji vipindi lilishangaa wakati watu wengi waipojitokeza na kusema kuwa wanaugua ugonjwa huo.

Image caption Mwanamume anayeugua mzio wa uso

Daktari Sarah Jarvis mtaalamu wa maswala ya kiafaya katika radio 2 ya BBC anasema kuwa mzio wa maji sio jambo la kawaida.

Baadhi ya watu wana mzio wa maji na kwamba hata jasho lao linaweza kusababisha kujikuna katika ngozi.

Muda ambapo ugonjwa huo humuathiri mwanadamu ni wakati wa kubalehe ,lakini pia unaweza kumuathiri mtu katika umri wowote ule maishani.

Nicola Branch, mwenye umri wa 51,kutoka London anasema kumekuwa na wakati ambapo unahisi kana kwamba kuna mtu amebeba kitu kinachokung'ata katika uso.

Ugonjwa huo unaosababisha kujikuna huathiri sana katika eneo la kisigino,nyuma ya magoti na uso.

Pia jasho husababisha mtu kujikuna.

''Nalazimika kubeba kitambaa cha mkononi ili kuweza kujifuta.Mara nyengine watu hawaamini kwamba una mzio.