Wanawake 'wanalewa sawa na wanaume'

Mvinyo Haki miliki ya picha Thinkstock

Wanawake wametoshana na wanaume katika kulewa, utaifiti wa kimataifa kuhusu mienendo ya kulewa unaonyesha.

Ukaguzi wa watu milioni 4 waliozaliwa kati ya mwaka 1891 na 2001, umeonyesha kuwa wanaume huedna wanalewa zaidi na kuugua matatizo ya kiafya.

Lakini kizazi cha sasa kimeziba pengo ripoti hiyo inasema.

Kubadilika kwa mienendo ya wanaume na wanawake katika jamiii ni sehemu ya ufafanuzi wa tofauti hiyo ya kulewa.

Utafiti huo unaonyesha kuwa watu waliozliwa mapema miaka ya 1900, wanaume:

  • Waliwazidi wanawake zaidi ya mara mbili katika kulewa
  • Walizidi kwa mara tatu uwezekano wa kulewa hadi kuingia katika matatizo
  • Na walikuwa katika uwezekano mara 3.6 zaidi kulewa hadi kuugua matatizo ya afya

Lakini kadrimiongo ilivyosogea, pengo lilifungwa kwa waliozaliwa mwishoni mwa karne na wanaume:

  • Walikuwa kiwango sawa kama wanawake katika kulewa
  • Walikuwa kiwango karibu sawa na wanawake cha 1.2 kulewa hadi kuingi katika matatizo
  • Pia walikuwa kiwango karibu sawa cha 1.3 na wanawake kuugua mataizo ya kiafya kutokana na kulewa

Wataalamu kutoka chuo kikuu cha New South Wales, nchini Australia, wamekagua data kutoka kwa watu kote dunani - licha ya kuwa uaguzi ulilengwa kwa ukubwa kueleka Amerika ya kaskazini na Ulaya.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Mtanagzo ya vile vinawalenga zaidi wanawake

Waliamua: "Kulewa na matatizo yanayotokanana kuelwa katika historia yametizamwa kama jambola wanaume.

"Utafiti huu sasa unazusha maswali kuhusu fikra hii na unaashiria kuwa wanawake, zaidi vijana ndio wanaopaswa kulengwa katika jitihada za kupunguza athari za vileo."

Prof Mark Petticrew, kutoka chuo cha London School of Hygiene and Tropical Medicine, amesema: "Majukumu ya wanawake na wanaume yamekuwa yakibadilika katika miongo - hili huenda ndio sababu ya kushuhudiwa mabadiliko haya, lakini sio yote.

"Uwepo wa rahisi wa mvinyo pia ni sababu kuu, kama ilivyo namna matangazo yanavyolenga zaidi wanawake na zaidi wanawake vijana.

"Wataalamu wa afya, ni lazima wausaidie umma - wanawake kwa wanaume - kuelewa hatari za afya katika kulewa, na namna y kupunguza hatari hizo."