Muongozo wa watoto wadogo kutazama vipindi

Sesame Street Elmo na Rosita

Chanzo cha picha, Getty Images / Sesame Street

Maelezo ya picha,

Sesame Street ni mojawapo ya vipindi vinavyopendekezwa watoto wadogo kutazama

Muungano wa madakatari wa watoto Marekani (AAP) umetangaza muongozo mpya kwa watoto walio na umri wa hadi miaka 2 kutazama TV.

Ulipendekeza kuwa watoto wa chini ya miaka 2 hawapaswi kutazama vipindi kwenye majukwaa yoyote.

Lakini sasa unasema watoto walio na umri wa zaidi ya miezi 18 yaani mwaka mmoja na nusu wanaweza kutazama chati za video na familia, na walio na umri wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitano wanaweza kutazama vipindi na wazazi wao.

Hatahivyo wamesisitiza kuwa ni muhimu kucheza na kuungumza ana kwa ana nao.

Chanzo cha picha, Thinkstock

Umetaja vipindi kama Sesame Street kama mfano wa vipindi vinavyofaa kutizamwa kwenye televisheni.

"Familia zinahitaji kutafakari namna watoto wao wanavyotizama yaliomo kwenye vyombo vya habari, na kuzungumza nao, kwasababu watoto kuzama sana katika hayo kutamaanisha kuwa hawana muda wa kutosha kucheza, kuosma na pia kulala kwa siku. Amesema Jenny Radesky, mwandishi mkuu wa ripoti ya muungano wa madaktari hao.

"Kilicho muhimu zaidi ni kuwa wazazi wanapaswa kuwaongoza watoto wao. Na hiyo inaa mana kuwafunza namna ya kutumia fursa hiyo katika kuwasiliana kujifunza na kuvumbua mambo."

Watoto walio na umri wa kati ya miaka 2 hadi miaka 5 wanapswa kuruhusiwa kutazama vipindi kwa saa moja kwa siku, Na wahudumu wanaowalea watoto hao wanapaswa kutenga muda wa hilo , inaongeza muongozo huo wa AAP.

Chanzo cha picha, Ronald Grant

Maelezo ya picha,

Watoto hujifunza zaidi kutokana na kusoma wanasaikolojia wanasema.

Ripoti hiyo inapendekeza kuundwa maeneo yasio na televisheni wala vyombo vingine vya kutazamaia vipindi nyumbani, mfano chumbani, kwa watoto wakiwemo wale wa zaidi ya miaka mitano.

Dr Catherine Steiner-Adair, mwanasaikolojia na mtafiti mwenza wa Harvard, ameiambia BBC kwama licha ya kuwa anapokea muongozo huo lakiniunahitaji ufafanuzi zaidi.

"Kuna haja kwa madakatri wa watoo kuwa wazi zaidi kuhusu watakachotizama watoto, vipindi vya kutazama na wazazi na kutazama huko kwa pamoja kuna maana gani," amesema.

"Unapotizama video na mtoto wa miaka 2 unataka kurejelea maneno kila mara, kuisimamaisha kwa muda video sawana tunavyofanya tunapowasomea watoto vitabu.

"Sio watu wawili waliokaa pamoja na kutazama kimya kimya."

Kipimo cha ufanisi

Dr Steiner-Adair ametaka utafiti zaidi pia katika ufanisi wa programu za watoto anazozitaja kuwa sekta 'isiyokaguliwa'.

"Ningependa kuona zaidi namna wanavyofanya ukaguzi wa mafunzo wanayopata watoto wa kati ya mwaka mmoja na nusu na miaka miwili na namna inavyolingana na kujifunza kwa kusomewa na mtu mzima kitabu."