'Upendeleo' katika kesi ya mke wa rais wa zamani Ivory Coast Simone Gbagbo

Simone Gbagbo Haki miliki ya picha AFP

Mawakili wa Simone Gbagbo, mke wa rais wa zamani wa Ivory Coast anayekabiliwa na kesi ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu , wametoka nje ya korti ya Abdijan inayosikiza kesi dhidi yake.

Wamekasirishwa na hatua ya mahakama kukataa kuwaruhusu kuwaita wanasiasa na maafisa wengine mashuhuri kama mashahidi katika kesi hiyo.

Ni pamoja na spika wa sasa wa bunge na aliyekuwa kiongozi wa waasi Guillaume Soro na aliyekuwa mkuu wa majeshi Philipe Mangou, gazeti la Jeune Afrique linaripoti.

Bi Gbagbo anatuhumiwa kwa kuhusika katika ghasia kubwa zilizojiri baada ya uchaguzi mkuu mnamo 2010.

Zaidi ya watu 3,000 aliuawa katika mpaigano yaliodumu miezi minne. Anakana mashtaka.

Alikuwa na ushaiwshi katika kambi ya kisiasa ya mumewe, rais wa zamani Laurent Gbagbo. Alikataa kukiri kushindwa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa urais kwa rais wa sasa Alassane Ouattara.

Kusikizwa upya kesi yake kuliahirishwa mara kadhaa kutokana na masuala ya mpango wa namna ya kuendesha kesi hiyo na ilianza wiki iliyopita tu.

Dohora Blede, Moja ya mawakili wanaomtetea Bi Gbagbo amenukuliwa na AFP akisema:

Tuna ahirisha kushiriki kwetu hadi tutakapoa taarifa baadaye. Kuna upendeleo katika kesi , mahakama haitaki kesi ya haki.

Tumegunuda kuwa mashahidi wetu hawako tumeomba kucheleweshwa kwa siku nne ili tuwaone watu hawa, ambao ni muhimu katika kudhihirisha ukweli."

Bwana Gbagbo ianakabiliwana kesi hivi sasa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kwa mashtaka kama hayo, ambayo anayakana.