Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Heathrow umeidhinishwa

Heathrow London Haki miliki ya picha Getty Images

Serikali ya Uingereza imeidhinisha kujengwa barabara yatatu ya ndege katika uwanja wa ndege wa Heathrow kuongeza kiwango cha shughuli katika uwanja huo Uingereza.

Mawaziri wameidhinisha uamuzi huo uliosubiriwa ka muda mrefu katika mkutano wa kamati ya bunge Jumanne.

Waziri wa uchukuzi Chris Grayling ametaja uamuzi huo "kuendana na wakati kikweli" na kusema upanuzi huo utaimarisha safari za Uingereza na mataifa mengine duniani na kusaidia kukuza biashara na nafasi za ajira.

Muungano wa wafanyakazi na makundi ya biashara yameafiki uamuzi wa kupanua uwanja wa ndege wa Heathrow.

Katibu mkuu wa TUC Frances O'Grady amesema ni "muhimu sana kwa Uingereza", huku mkuu wa CBI Paul Drechsler amesema itsaidia kuunda nafasi za ajira na kushinikiza ukuwaji wa uchumi.

Maafisa wasimamizi wa Heathrow wanasema uwanja huo upo tayari kujenga njia ya tatu ambayo "haitogharimu fedha nyingi na itakayohakikisha kupatikana faida zinazotazamiwa kwa Uingereza nzima".

Hatahivyo, Sadiq Khan, meya wa mji wa London, amesema ni uamuzi usio faa kwa London na Uingereza kwa jumla.

Kupanua uwanja huo kusini mashariki mwa England imekuwa ni karata ya kisiasa kwa miaka mingi.

Licha ya kuwa uwanja huo wa Heathrow unapendelewa zaidi katika biashara, umevutia upinzani mkubwa kutoka kwa wabunge wa maeneo yalio karibu na uwanja huo na njia za ndege kupita.

Zac Goldsmith, mbunge wa chama cha Tory Richmond Park aliyetishia kujiuzulu iwapo upanuzi huo wa Heathrow utaihinishwa, ametaja tangazo hilo kama "janga" na amesema atakutana na wakaazi anaowawakilisha kabla ya kutoa taarifa baadaye Jumanne.

Waziri wa mambo ya nje Boris Johnson na waziri wa elimu Justine Greening pia wamepinga upanzui wa uwanja wa ndege wa Heathrow.