Mateka walioachiliwa Somalia wahofia maisha huru

Mateka walioachiliwa Somalia wahofia maisha huru

Utaanzaje maisha yako upya baada ya kuishi kizuizini kwa zaidi ya miaka minne? Hii ndio changamoto inayowakabili mabaharia 26.

Waliachiliwa Jumamosi na maharamia wa Kisomali baada ya kuteka nyara meli yao mwaka wa 2012. Mabaharia hao, hasa kutoka mataifa ya kusini mwa Asia sasa wanajiandaa kurudi nyumbani.

Kisa chao kinafufua ukatili wa uharamia katika pwani ya bahari Hindi ambao kwa muda ulisahaulika.

Mwandishi wa BBC Dayo Yusuf alikutana nao jijini Nairobi.