Mazungumzo ya sekunde 30 yanayoweza kukupunguza uzani

Ukaguzi wa uzani wa watu walio na uzani wa juu kupitia kiasi
Image caption Ukaguzi wa uzani wa watu walio na uzani wa juu kupitia kiasi

Madaktari wanaotumia sekunde 30 wakiwaambia wagonjwa kwamba wanahitaji kupoteza uzani wanaweza kuwa na athari kubwa ,utafiti unaonyesha.

Watu kadhaa ambao hawakuwa na lengo la kupunguza uzani ,walipoteza asilimia 10 ya uzani wa mwili wao baada ya kupewa mpango wa bila malipo wa kupunguza uzani.

Chuo kikuu cha watafiti wa Oxford kinasema kuwa mazungumzo ya sekunde 30 yangekuwa na athari kubwa iwapo kila mgonjwa angefanya.

Matokeo hayo ,yaliochapishwa katika jarida la Lancet ,yalionyesha kwamba wagonjwa hawakukosewa na ushauri huo.

''Daktari wako anaweza kuzua swala la uzani wako,sio kama kumwambia mkeo ana uzani wa juu kupitia kiasi'',alisema Paul Cooper ambaye alishiriki katika majaribio.

Alikuwa anaenda kumuona daktari wake kama kawaida hadi pale daktari huyo alipomwambia kwamba uzani wa kilo 98 sio mzuri kwa afya yake.

''Nikiangalia chini'',sikuweza kuona miguu yangu alisema mtu huo mwenye umi wa miaka 69.

Paul alikuwa miongoni mwa watu 2,728 walio na uzani wa kupita kiasi walioshiriki katika ukaguzi huo.

Wote walikwenda hospitalini kumuona daktari kwa maswala mengine ya kiafya wakati daktari huyo aliposema hivi: Wakati muko hapa ningependa kuzungumza kuhusu uzani wenu.

Nusu ya idadi hiyo walipewa ushauri wa kupunguza uzani.

Ni wanne kati ya 10 waliotekeleza ushauri huo ,huku robo ya wagonjwa hao wakipoteza asilimia 5 ya uzani wao na takriban moja ya kumi wakipoteza asilimia 10 wa uzani wao baada ya mwaka mmoja.