Forbes: Rais Magufuli kuwania tuzo la mtu mashuhuri

Rais Magufuli kuwania tuzo la Forbes la mtu mashuhuri wa mwaka
Image caption Rais Magufuli kuwania tuzo la Forbes la mtu mashuhuri wa mwaka

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania tuzo la Forbes la mtu mashuhuri wa mwaka.

Jarida hilo la biashara limemtambua rais Magufuli kwa umuhimu wake katika kuimarisha uchumi wa taifa hilo.

Wengine walioteuliwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na Benki ya Capitec nchini Afrika Kusini,rais wa Mauritania,Mtetezi wa haki za umma nchini Afrika Kusini na raia wa Rwanda.

Mwaka uliopita tuzo hilo lilichukuliwa na mfanyibiashara wa Tanzania Mohammed Dewiji.