Wasanii Sudan kusini wachora kushinikiza amani Juba
Baada ya vita vya takriban miaka mitatu, wasanii Sudan kusini wameshirikiana katika kujaribu kuishinikiza nchi kukaa pamoja na kujadili amani, kwa kuanzisha michoro katika maeneo ya umma mjini Juba.

Chanzo cha picha, Ana Taban
Kuta na mabohari yamechorwa kote mjini

Chanzo cha picha, Ana Taban
Mkusanyiko wa michoro ya Ana Taban (kutoka neno la kiarabu "nimechoka") linatokana na jina la vuguvugu la kuunga amani mkono Syria.

Chanzo cha picha, Ana Taban
Michoro hiyo inaangazia mateso ya watoto katika vita vya kiraia. "mwishowe wao ndio watakaolazimika kukusanya kilichosalia na kuunganisha upya Sudan kusini," kundi hilo linasema.

Chanzo cha picha, Ana Taban
Kuta za shule taasisi za kitamaduni Juba zimepambwa kwa michoro ya wasanii hao.

Chanzo cha picha, Ana Taban

Chanzo cha picha, Ana Taban
Takriban watoto milioni moja wameachwa bila makaazi , jambo lililoliharibu taifa ambalo lilikuwa na matumaini makubwa wakati wa uhuru wake miaka itano iliyopita, lilipokuwa taifa changa duniani.

Chanzo cha picha, Ana Taban
Abul Oyay Deng ni mwanafunzi aliyetoroka vita mnamo 2013, na kuishia Nairobi, lakini amerudi nyumbani kujiunga na mradi huo.

Chanzo cha picha, Ana Taban
Wasanii hao wameshirikiana na wakaazi wa mitaa ya karibu katika baadhi ya michoro.

Chanzo cha picha, Ana Taban
Mwanamume aliyechorwa akionekana anamtibu mtoto ni mfano wa Dr. Ding Col Dau, alierudi Sudan kusini mnamo 2014 kutoa huduma ya afya lakini aliuawa nyumbani kwake mwaka uliofuata.

Chanzo cha picha, Ana Taban
Tunakata mizizi yetu, tunajiangamiza - inangazia taswira ya mizozo inavyoharibuna kuathiri jamii.

Chanzo cha picha, Ana Taban
Kampeni ya kwenye mtandao #SaveTheLastTrain na mshairi Akol Miyen, ndiyo ilishinikiza mchoro huu. "Hii ndio treni ya mwisho kwasababu nafasi yetu kama taifa zinamalizika," kundi hilo linasema.
Baada ya kusambaza ujumbe wake katika baadhi ya kuta za mji wa Juba, kundi hilo sasa linapanga kupanua mradi wake nje ya mji mkuu huo.