Korea Kaskazini 'haiko tayari kuziacha' silaha za nyuklia

Waangalizi wanasema Korea kaskazini wamepiga hatua katika kutengeneza makombora Haki miliki ya picha KCNA
Image caption Waangalizi wanasema Korea kaskazini wamepiga hatua katika kutengeneza makombora

Sera ya Marekani kuishawishi Korea kaskazini kuachana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia huenda 'haina ufanisi' , mkurugenzi wa shirika la kitaifa la ujasusi Marekani amesema.

James Clapper amesema Marekani jambo ambalo Marekani inaweza kutumainia ni kuzuia uwezo wa taifa hilo, katika hotuba New York.

Ni nadra kwa Marekanikukiri kuwa lengo lake kuu la kuwa na dunia isiyokuwana matumizi ya nyuklia huedna isifanikiwe.

Hatahivyo, wizara ya mambo ya nje Marekani inasema sera yake hiyo haijabadilika.

Korea kaskazini inadai kupiga hatua katika mradi wake wa kutengeneza silaha za nyuklia licha ya upinzani wa kimataifa na vikwazo vikali.

Mnamo Septemba, ilifanya jaribio lake la tano na kubwa la silaha zake za nyuklia, jambo lililozusha shtuma kote duniani.

Akizunguma katika baraza kuhusu uhusiano wa nchi za nje siku ya Jumanne, Clapper ameitaja serikali ya KOrea kaskazini kama iliyo na 'uoga' na kusema inaona silaha za nyuklia kama 'tikiti yao ya kuendelea kuwepo'.

Amependekeza, kutoa vikwazo vya kiuchumi kwa kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un kupunguza silaha zake za nyuklia huenda ndio sera bora zaidi.

Haki miliki ya picha Geoeye
Image caption Kinu cha nyuklia cha Korea huko Punggye-ri ndiko majaribio ya silaha hizo yalikofanyika

Akijibu kauli ya Bwana Clapper, wizara ya mambo ya nje imesema bado inanuia kufanya majadiliano ya mataifa sita, ambayo Korea kaskazini ilijitoa mnamo 2009.

Marekani inatarajia kutuma mfumo wake wa ulinzi wa anga za juu Korea kusini (THAAD) hivi karibuni, licha ya upinzani kutoka China na Korea kaskazini.

Washington na Seoul zinasisitiza ni kwa lengo la kuimarisha ulinzi tu dhidi ya tishio kutoka kwa Korea kaskazini.