Meli za kivita za Urusi 'kukwepa' Uhispania

Admiral Kuznetsov Haki miliki ya picha EPA
Image caption Admiral Kuznetsov, ambayo ina uwezo wa kubeba ndege nyingi za kivita, tayari imefika katika pwani ya Syria

Manowari za Urusi, ambazo zilikuwa zimetarajiwa kusimama Uhispania kuongeza hazina ya mafuta, hazitasimama nchini humo tena kutokana na wasiwasi wa mataifa wanachama wa Nato.

Urusi inaripotiwa kuondoa ombi lake la kutaka meli hizo za kivita zitie nanga katika bandari ya Cueta.

Wizara ya mambo ya nje ya Uhispania amekiri kwamba meli hizo hazitasimama katika pwani yake.

Uhispania imekuwa ikishinikizwa na mataifa wanachama wa shirka la kujihami la nchi za Maghafibi, Nato, kutoruhusu meli hizo zinazoelekea Syria kuongezwa mafuta kwenye bandari zake.

Kundi la meli za kivita za Urusi zimekuwa zikielekea bahari ya Mediterranean kusaidia kutekeleza mashambulio dhidi ya waasi wanaopinga Rais Bashar Assad.

Urusi ilikuwa awali imepewa ruhusa ya kuingiza meli tatu bandari ya Cueta kati ya 28 Oktoba na 2 Novemba.

Nato imekuwa ikipinga mashambulio yanayotekelezwa na Urusi nchini Syria, na inahofia meli hizo zitatumiwa kuzidisha mashambulio dhidi ya maeneo yenye raia Aleppo.


Haki miliki ya picha EPA
Image caption Meli hizo zinatarajiwa kupitia Mlango wa Bahari wa Gibraltar baadaye Jumatano

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii