Nyota ya Donald Trump Hollywood yaharibiwa

Donald Trump's star Haki miliki ya picha Twitter/NBC

Nyota ya mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump katika Hollywood Walk of Fame imeharibiwa na mtu aliyekuwa na nyundo kubwa.

Mwanamume huyo alionekana akiiharibu nyota hiyo Jumatano jioni.

Waandishi wa habari wanasema mwanamume huyo alitaka kuipiga mnada kuchangisha pesa za kusaidiwa wanawake ambao wanadai Bw Trump aliwadhalilisha kimapenzi.

Mgombea huyo amekanusha madai hayo na kusema ni uongo mtupu.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mgombea huyo alipewa nyota hiyo mwaka 2007 kutokana na utangazaji wake katika kipindi cha Apprentice.

Hii si mara ya kwanza kwa nyota hiyo kuharibiwa.

Miezi michache iliyopita, ukuta wa mfano uliwekwa kuzunguka nyota hiyo baada yake kutangaza kwamba angejenga ukuta mpakani wa Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji wasiingie Marekani.

Haki miliki ya picha AP