West Ham watimua Chelsea Kombe la EFL

Ulikuwa mwanzo mbaya wa West Ham kutumia uwanja wa London Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ulikuwa mwanzo mbaya wa West Ham kutumia uwanja wa London

West Ham wamefika hatua ya robo fainali Kombe la EFL baada ya kudhihirisha ubabe wao na kuwalaza Chelsea kwenye mechi iliyochezewa uwanja wa London, zamani ukijulikana kama uwanja wa Olimpiki.

Mechi hiyo hata hivyo ilikumbwa na vurugu za mashabiki.

Chupa za plastiki na viti vilirushwa mamia ya mashabiki walipokabiliana karibu na mwisho wa mechi.

Cheikhou Kouyate alifunga bao la kichwa kabla ya muda mapumziko, naye Edimilson Fernandes akaongeza la pili dakika chache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.

Gary Cahill alikomboa bao moja dakika za mwisho mwisho lakini lilikuwa tu la kufutia machozi.

West Ham watakutana na Manchester United ambao walilaza Manchester City 1-0 kwenye mechi nyingine iliyochezwa usiku wa Jumatano.

Southampton nao walilaza Sunderland 1-0.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Polisi wa kupambana na fujo walitumwa kudhibiti mashabiki
Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption John Terry alirejea uwanjani kwa mara ya kwanza tangu alipocheza dhidi ya Swansea tarehe 11 Septemba

West Ham mechi yao ijao itakuwa dhidi ya Everton uwanjani Goodison Park ligini tarehe 30 Oktoba nao Chelsea siku hiyo wame ugenini St Marys dhidi ya Southampton.