Waziri mkuu anayeongoza kupitia picha yake

Picha ya waziri mkuu Jayaram Jayalalitha mbele ya mkutano wa baraza la mawaziri
Image caption Picha ya waziri mkuu Jayaram Jayalalitha mbele ya mkutano wa baraza la mawaziri

Ni vipi Waziri mkuu anayeugua wa Tamil Nadu Jayaram Jayalalitha anaendelea kutawala jimbo hilo la Kusini mwa India?.

Amekuwa hospitalini tangu tarehe 22 mwezi Septemba na wasiwasi kuhusu afya yake umeenea kutokana na ukosefu wa habari kuhusu hali yake.

Chama chake cha AIADMK ambacho kinaongoza jimbo hilo,hivi majuzi kilitangaza kwamba kimehamisha majukumu yake yote kwa naibu wake OP Pannerselvam,ambaye alimuunga mkono katika siku za nyuma.

Hatahivyo iliwekwa wazi kwamba atasalia waziri mkuu.Kwa hivyo ni vipi baraza lake la mawaziri linakutana bila yeye.

Wanaonekana kupata suluhu ya picha yake.

Picha yake rasmi iliotolewa na serikali ya jimbo hilo inamuonesha Panneerselvam katika mkutano wa baraza la mawaziri akiwa na picha ya Jayalalitha mbele yake.

Image caption Picha ya waziri mkuu ikiwa katika mkutano wa wizara ya kilimo huko Tamil Nadu

Na sio mikutano ya baraza la mawaziri pekee ambapo pia hiyo huwekwa.

Picha hiyo pia huwekwa mbele ya mikutano ya wizara kadhaa.

Panneerselvam alimsimamia waziri huyo mkuu katika hafla mbili wakati alipokuwa jela kwa madai ya ufisadi,lakini hakuchukua mahala pake.

Aliamua kwamba hatoketi katika kiti chake,kwa kuwa anahisi bado anashikilia wadhfa huo.

Alipendelea badala yake kufanya mikutano yake akiwa ameketi katika kiti mwisho wa meza.