Makanisa yaunga mkono uavyaji mimba Malawi

Makanisa nchini malawi yaunga mkono uavyaji mimba
Image caption Makanisa nchini malawi yaunga mkono uavyaji mimba

Baraza la makanisa nchini Malawi limeambia kipindi cha BBC focus on Africa kwamba linaunga mkono marekebisho katika sheria ya uavyaji mimba itakayoruhusu hatua hiyo kutekelezwa kwa misingi fulani.

Misingi hiyo ni iwapo afya ya mama ipo hatarini,mimba inayotokana na ubakaji,kujamiana kwa watu wa familia moja na unajisi.

Baraza hilo la MCC ambalo ndio muungano mkubwa zaidi wa makanisa ya katholiki na Protestant umesema kuwa unaunga mkono mabadiliko hayo kutokana na idadi kubwa ya wanawake wa Malawi wanaofariki katika jaribio la kuavya mimba kwa kutumia njia zisizo salama.

Hatahivyo katibu mkuu Gilford Matonga amesema kuwa MCC bado inapinga uavyaji mimba unaofanywa bila msingi.