Maduro aongeza asilimia 40 katika mishahara

Maduro Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Nicolas Maduro

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameongeza asilimia arobaini katika mshahara wa chini, hiyo ikiwa ni nyongeza ya nne mwaka huu.

kupanda huko kunakuja siku moja baada ya maelfu ya watu walioingia mitaani kupinga serikali.

Maduro alitangaza kuongeza huko katika hotuba yake kwa umma nchini humo.

Nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta inakumbana upungufu wa chakula na kuporomoka kwa uchumi. Maandamano makubwa yanaendelea ili kumshinikiza Rais Maduro kuondoka madarakani, na viongozi wa upinzani wameitisha maandamano mengine ya umma siku ya leo.