ELN:tutaachia mateka nchini Colombia

Santos Haki miliki ya picha Empics
Image caption Rais wa Colombia Juan Manuel Santos

mpatanishi mkuu wa serikali ya Colombia kwenye makubaliano ya amani na waasi wa ELN amesema wameanza mchakato wa kuwatoa mateka ambayo ni hatua muhimu kwa ajili ya kuanza mazungumzo rasmi ya amani.

Juan Camilo Restrepo ambaye ni mpatanishi amesema kuwa taarifa zimetolewa na shirika la msalaba mwekundu.

Mazungumzo na waasi wa mrengo wa kushoto yanatarajiwa kuanza leo katika mji mkuu wa Ecuado, Quito. Lakini rais wa Colombia Juan Manuel Santos amesimamisha muda wa mazungumzo kabla ya kuanza na kusema kuwa mbunge wa zamani wa bunge la nchi hiyo Odin Sanchez, awe wa kwanza kuachiwa mateka na waasi hao.