Mahangaiko ya familia ya Mkenya aliyefungwa Guantanamo
Huwezi kusikiliza tena

Mahangaiko ya familia ya Mkenya aliyefungwa Guantanamo

Wakati uongozi wa rais Barrack Obama wa Marekani unakaribia kumalizika, dosari kubwa iliyotia doa uongozi wake ni kushindwa kulifunga gereza la Guantanamo kama alivyoahidi.

Gereza hilo limeshutumiwa kuendeleza mateso na ukiukwaji wa haki za binadamu katika harakati za vita dhidi ya ugaidi.

Athari zake zimesambaa hadi Afrika Mashariki. Jijini Mombasa familia ya mtu mmoja ambaye amefungwa huko Guantanamo kwa zaidi ya miaka tisa imekuwa ikihangaika katika juhudi zake za kutakata aachiliwe huru.

Ferdinand Omondi ana taarifa hiyo kutoka Mombasa.