NATO; hatutaki mzozo na Urusi

Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg.

Nato haitafuti mzozo na Urusi wala haihitaji vita vingine baridi kwa mujibu wa katibu mkuu wa jumuiya hiyo, Jens Stoltenberg.

Stoltenberg anasema kuwa mipango ya kupeleka wanajeshi 4000 zaidi mashariki mwa Ulaya ina lengo la kuzuia badala ya kuzua mzozo.

Licha ya kuwepo misukosuko, muungano wa Nato hautambui Urusi kuwa tisho.

Uhusiano kati ya nchi za magharibi na Urusi umekuwa mbaya zaidi tangu vimalizike vita baridi.

Marekani na Muungano wa Ulaya walikuwa wameiwekea Urusi vikwazo kufuatia hatua yake ya kuimega rasi ya Crimea mwaka 2014.

Image caption Rais wa Urusi Vladimir Putin

Vita ncchini syria navyo vimeluwa chanzo cha misukosuko, huku mataifa mnakubw ayaliilaju Urusi wa kuendsha uhalifu wa kivita inapioshgambualia ameneoa yanayodhibitiwa na uopiannai ikiisadia serijali.

Vikosi vya kimataifa vinavyo jumuisha wanajeshi 1000 katika kila kikosi vitapelekwa nchini Poland, Latvia na Lithuania mapema mwaka ujao.

Vikosi hivyo vitaongozwa na Marekani, Uingereza, Canada na Ujerumani.

Nato inasema inaamini kuwa Urusi ina takriban wanajeshi 330,000 walioa karibu na mashariki ya mpaka wake.

Mapema wiki hii mipango ya meli za kivita za Urusi kutia nanga katika bandari ya Uhispania ilivutwa baada ya washirika wa Nato kuelezea wasi wasi kuwa zitatumiwa kushambulia raia nchini Syria.