Mashindano ya ulaji nyama kufanyika Zimbabwe

Mashindano ya ulaji nyama kufanyika Zimbabwe Haki miliki ya picha AP
Image caption Mashindano ya ulaji nyama kufanyika Zimbabwe

Watu nchini Zimbabwe wanajiandaa kuvunja rekodi ya kula nyama nyingi zaidi ya kuchomwa au braai jinsi inavyojulikana nchini humo.

Katika warsha hiyo inayodhaminiwa na kinywaji cha Castle Lager, mipango itakuwa ni kula tani 10 za nyama choma siku ya Jumamosi katika klabu moja iliyo mjini Harare.

Ukurasa wa kampuni mfadhili wa Facebook una video za kuwashauri watu kufika na pia imetangaza kupitia mtandao wa Twitter.

Mapema mwaka huu Rais Robert Mugabe alitangaza janga la kitaifa katika maeneo ya vijijini yaliyokumbwa na ukame.

Inakadiriwa kuwa watu milioni 2.4 kwa sasa wanahitaji msaada wa chakula ikiwa ni zaidi ya wa robo ya watu wote nchini Zimbabwe.