Athari za ukame nchini Zimbawe

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabwawa yanazidi kukauka nchini Zimbabwe

Ukame nchini Zimbabwe kimeacha bwawa kubwa zaidi nchini humo la Kariba na asilimia 9 tu ya maji ikiwa imesalia, kwa mujibu wa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa

Akizungumza alipokuwa akizindua mpango wa kupambana na ukame, bwana Mnangagwa alisema kuwa kwa ujumla mabwawa yote ya nchi hiyo yana asilimia 42 ya maji.

Ukosefu wa mvua mapema mwaka huu uliosabababishwa na msimu wa El Nino ulichangia mamilioni ya watu kukoso chakula na Rais Robert Mugabe ametangaza hali ya hatari katika maeneo kadha nchini humo.