Wanyama watoroka mbuga kwa sababu ya kiangazi Kenya

Wanyama watoroka mbuga kwa sababu ya kiangazi Kenya

Nchini Kenya hali ya kiangazi iliyoko nchini humo imesababisha muingiliano kati ya wanyama wa pori na binadamu baada ya wanyama hao kukosa maji na chakula katika mbuga zao na kulazimika kuvamia mashamba.

Kati ya sehemu zilizoathiriwa ni wilaya ya Tana River ambapo kuna wakulima wanaohangaishwa sana na tumbili (ambao wanawaita Mayonda) na ngiri.

Mwandishi wetu Bashkas Jugsodaay alitembelea shamba moja na kukutana na mkulima Mohamed Mathoya.