Wanamgambo wa Shia walenga kuukomboa mji wa Tal Afar, Mosul

Wanamgambo wa madhehebu ya Shia wanasema wanalenga kuukomboa Tal Afar Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES
Image caption Wanamgambo wa madhehebu ya Shia wanasema wanalenga kuukomboa Tal Afar

Makundi ya wanamgambo wa madhehebu ya Kishia yanasema yameidhinisha shambulio dhidi ya wanamgambo wa Islamic State magharibi mwa mji wa Mosul, wakati mapigano ya kuudhibiti upya mji huo yakiendelea.

Makundi ya Hashid Shaabi yanasema lengo lao ni kulitoa kundi la IS kutoka mji wa Tal Afar, na kuziba njia za wapiganaji hao wa jihadi kuelekea Mosul kutoka Syria.

Mji wa Tal Afar una idadi kubwa ya madhehebu ya Shia kabla ya IS kuuteka mnamo 2014. Mosul nao ni mji wenye Madhehebu ya Sunni na wanamgambo wa Shia wameapa kutoingia mji huo.

Wakati huo huo kundi la Hezbollah brigades, la wanamgambo wa kishia Iraq limesema linashiriki katika mashambulio hayo pia dhidi ya kundi la IS huko magharibi mwa mji wa masol.

Wamesema wanakaribia mji wa Tal Afar wakishirikiana na makundi mengine.

Serikali ya Iraq ikisaidiana na wapiganaji waki-kurdi ilianzisha mashambulio mengine makali dhidi tangu wiki jana nyenye lengo la kuirudisha mji wa Mosul mikononi mwa serikali.

Majeshi ya Marekani yanawashambulia IS kwa ndege za kivita.