Kila unachohitaji kujua kuhusu uchaguzi Marekani

Kituo cha kupiga kura 2012 Haki miliki ya picha Getty Images

Mnamo Januari 2017, taifa lenye nguvu duniani litakuwa na kiongozi mpya baada ya kampeni ndefu tena iliyokuwa ghali - lakini uchaguzi wa Marekani unakuwaje?

Marekani inapochagua rais, haichagui kiongozi wa taifa na mkuu wa amiri jeshi kubwa duniani.

Ni jukumu kubwa sana. Kwahivyo mpango unakuwaje?

Nani anayeweza kuwa rais?

Kiufundi kuwania urais , sharti uwe mzaliwa Marekani, raia, mwenye umri usiopungua miaka 35 na uwe umeishi nchin ikwa miaka 14.

Inaonekana rahisi sio?

Hatahivyo kwa kweli, karibu marais wote tangu 1933 wamewahi kuwa magavana, seneta au mwanajeshi wa kiwango cha juu. Na hilo ni kabla ufikirie iwapo utateuliwa katika chama na kuvutia vyombo vyahabari kitaifa.

Katika uchaguzi mwaka huu 2016 katika kiwango kimoja ambapo kulikuwa na magavana 10 au waliokuwa magavana na kumi waliokuwa masentea au waliokuwa katika wadhifa huo, hatahivyo wengi walijitoa.

Mtu mmoja anateuliwa kuwa mgombea wa chama cha Republican na Democratic katika uchaguzi.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kwanini ni Hillary Clinton v Donald Trump?

Msururu wa uchaguzi unafanyika katika kila jimbo na maeneo ya ng'ambo, kuanzia Februari, unaobaini ni nani anayekuwa mgombea rasmi wa kila chama.

Kila mshindi anakusanya idadi ya wajumbe - ambao ni wanachama walio na mamlaka ya kumpigia mgombea kura katika mkutano wa chama uliofanyika Julai ambapo wagombea walithibitishwa rasmi.

Democrat Hillary Clinton mwanachama wa Republican Donald Trump walikuwa washindi wa wazi mwaka huu na waliteuliwa rasmi katika mikutano ya vyama vyao.

Waliwateua pia wanaonuia kuwa makamu wao wa rais - Senata Tim Kaine kutoka Virginia kwa Bi Clinton, na Gavana wa Indiana Mike Pence kwa chama cha Republican.

Sera kuu katika kampeni

Kumekuwa na msururu wa mzozo ulioanzishwa na Donald Trump, tangu mfanyabiashara huyo alipozindua kampeni yake kwa kuwataja wahamiaji wa Mexico kama 'wabakaji na wahalifu'. Ugombea wake umekumbwa na mzozo kila wiki kadha zinapopita. Amezusha mzozo wa maneno na jaji, mwanamitindo wa zamani na familia ya kiislamu ya mwanajeshimmoja aliyeuawa vitani.

Amelazimika kutetea kukaidi kwake kuwasilisha malipo yake ya kodi na pendekezo kwamba huenda hajalipa kodi kwa miaka 18 na pia kutetea maswali yanayozuka kuhusu shirika lake la misaada.

Na Hillary Clinton amekabiliwa na shutuma kivyake. Mzozo kuhusu barua pepe binafsi alizotuma zimetia dosari heshima yake kwa kiwango kizito,na kumekuwa na maswali kuhusu misaadaya nje wanayotoa kupitia wakfu wao familia yake - Clinton Foundation. Trump pia ameangazia kuhusu jukumu lake katika kuwanyanyasa wanawake waliodai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe Bill. Na mtandao wa WikiLeaks umekuwa ukifichua barua pepe zilizovamiwa katika mtandao zilizodhihirisha mawasiliano ya aibu kai ya wafuasi wa timu yake ya kampeni.

Haki miliki ya picha Getty Images

Ni nani aliyeshinda mjadala wa tatu?

Awali wagombea walijadili sera lakinimjadala ukapamba moto wakati Bi Clinton alipogeuza suali kuhusu Wikileaks kuwa shambulio dhidi ya uhusiano wa Trump na Urusi.

Wakati huo Trump wa kukatiza kauli akarudi na kuanza kumuita Bi Clinto mrongo na kudai kwamba yeye ndio kinyago cha Urusi na sio yeye.

Trump amesema wanawake wanaomshutumu kuwanyanyasa kingono, aidha ni watu wanaotaka kujulikana au wafuasi wa kampeni ya Clinton.

Donald Trump alikataa kuahidi kukubali matokeo ya uchaguzi iwapo atashindwa, katika mjadala wa mwisho wa urais dhidi ya Hillary Clinton Las Vegas.

"Nitakuambia wakati huo," alimwambia muendesha mjadala Chris Wallace.

Kwa siku kadhaa amedai kuwa kuna 'udanganyifu' katika uchaguzi huo.

Ni kauli iliyosalia kwenye vichwa vya habari na kugubika majadiliano kwa siku kadhaa.

Uchaguzi wa Novemba unakuwaje?

Kura zinapigwa Jumanne Novemba 8.

Mgombea mwenye kura nyingi katika kila jimbo anakuwa mgombea anayeungwa mkono katika jimbo hilo kuwa rais.

Yote itaishia katika mpango wa uchaguzi uanojulikana kana the electoral college, kundi la watu 538 watakao mchagua rais . Na nusu ya idadi hiyo inatosha kumchagua rais.

Lakini mjimbo yote hayako sawa - California, kwa mfano ina zaidi ya mara 10 idadi ya atu wa Connecticut, kwahivyo kuna tofauti ya uzito.

Kila jimbo ina idadi yake ya wapiga kura hao kutokna na idadi ya watu katika jimbo.

Wakati raia wanapomchagua mgombea wanaompendelea, wanawachagua pia wapiga kura hao.

Lakini katika karibu kila jimbo (isipokuwa Nebraska na Maine), mshindi huchukua kura zote - kwa hivyo mtu anayeshinda wapiga kura wengi mfano New York, for example, atapata kura zote 29 zinazopigwa New York.

Haki miliki ya picha Getty Images

Rais anaanza kazi lini?

Siku na wiki kadha baada ya uchaguzi - iwapo kura zitaamua - mshindi ataunda baraza la mawaziri na ataanza kuunda sera kamilifuya uongozi.

Wakati huo huo rais anayeondoka anajitahidi kuacha sifa nzuri ya uongozi wake na kufungasha virago vyake.

Kwa mujibu wa katiba ya Marekani, rais anaapishwa Januari 20 ya mwaka unaouata uchaguzi ulipofanyika.